Makahaba wazee wa Korea Kusini

Haki miliki ya picha BBC World Service

Wazee katika baadhi ya nchi huheshimika na kuwa akiba ya busara kwa kizazi cha vijana na zaidi ya yote huangaliwa na kusaidiwa kimaisha.

Huko nchini Korea Kusini maisha kwa wazee ambao walichangia katika uchumi wa taifa hilo na ustawi wa taifa hivi sasa wanaishi katika mazingira magumu hali ambayo kwa wanawake wazee inawalazimu kubuni mbinu mpya za maisha kwa kujitumbukiza katika biashara haramu ya ngono kwa kuuza miili yao ili waweze kujipatia fedha za kuendesha maisha yao ya kila siku.

Katika nchi zilizo nyingi na hata Afrika mashariki biashara ya ngono hufanywa na wasichana wadogo.

Akiwa amevalia koti lake jekundu,na kupaka rangi ya mdomo kwa ustadi Bi. Kim Uen Ja mwenye umri wa miaka 71 mavazi yake yanabainisha wazi kwamba angependa kuwa na muonekano wa msichana mdogo na mrembo, yupo katika eneo la kupumnzika la Jongno-3 subway station huku pembeni mwake akiwa na begi kubwa lililosheheni chupa ndani yake.

Bi. Kim ni mmoja kati ya wanawake wazee wa Korea ya kusini ambao hupendelewa kuuza kinywaji ambacho wanaume wanasema kinawaongezea nguvu kijulikanacho kwa jina la Bacchus, lakini wanawake hawa wanaouza vinywaji hivi baadhi yao ni wale wenye malengo ya kujiuza ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.

'Siwezi kuwategemea watoto wangu kunisaidia katika maisha, kwa sababu wapo katika matatizo kwani wanapaswa kuanza kujiandaa kukabiliana na maisha yao ya siku za uzee wao,anasema Bi.Kim.

"Unaona wanawake wote waliosimama pale?anauliza, wote hao wana biashara nyingine zaidi ya kinywaji hiki Bacchus, kuna wakati wanakwenda na wazee hao wakiwa wamewanunua kimapenzi na wanajipatia fedha nyingi toka kwao,japo mimi siishi kama wao anawabeza.

Mwanamke huyu mzee akielezea mapato yake anasema hupata hadi dola tano kwa siku ama paundi tatu,kwa kuuza kinywaji chake kwa mfumo wa haraka haraka mwenyewe akiuita 'drink up fast.'

''Polisi muda wote hunishangaa ninavyofanya kazi zangu,'' anasisitiza mwanamke huyu.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Mwandishi wa BBC Lucy Williamson alitembelea eneo la uwanja wa michezo anasema alikuta kundi la wanaume wazee wakipata kinywaji chao huku kukiwa na wanawake wazee wengi pia.

''Sisi ni wanaume bwana na tunapenda wanawake,tunapata kinywaji,kiasi kingine cha fedha tunawapa hawa wanawake kwaajili ya kuwapata kimapenzi, kisha akacheka kidogo na kumalizia kwa kusema na kwa hakika tunawapata, na kwetu haijalishi ati ni wazee sana ama hawana msisimko wa kimapenzi hilo si tatizo''alisema mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 60.

"Tunaweza kupata marafiki wa kike hapa si unawaona wale wanawake waliosimama pale? Wapo pale wakihitaji tuwalipe kasha twende nao,gharama ya kuwapata ni kati ya paundi 11 hadi 17 lakini wakati Fulani kunakuwa na punguzo wanakubali tu''anasema mwanaume mwingine mwenye miaka 81 hivi.

'Nina hasira, tena hasira kali, sihitaji heshima yoyote, ninachohitaji ni kupata chakula mara tatu kwa siku'anasema mwanamke mzee anayejiuza.

Serikali inafanya jitihada kukomesha hali hiyo japo kuwa raia hao hawana akiba ya fedha,bima ya maisha ama malipo kwaajili ya kuwasaidia wazee hali inayowafanya kushindwa kujitegemea.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Michoro kwenye kuta za mji wa Seoul

Hata hivyo kuwategemea watoto wao wanawake hawa wanasema ni jambo la upuuzi,"wale wote wanaowategemea watoto wao ni wajinga kizazi chetu kilikuwa cha heshima,tuliwaheshimu na kuwasaidia wazazi wetu, lakini kizazi cha sasa kinajiona cha wasomi na kudharau wazazi''anasema Bi Kim.

Polisi ambao wamekuwa wakiendesha doria kuwasaka wanawake hao wanaojiuza wanasema tatizo hili ni kubwa na kwamba hawadhani kama linaweza kukomeshwa kkwa urahisi ati kwa kuwaweka chini ya ulinzi bali sera kwa ujumla inapaswa kubadilika.

Hata hivyo kwa wale wanaobainika na kupekuliwa katika mabegi yao wanakutwa na sindano ambazo wanawake hao huwadunga wanaume kwenye mishipa ili kusisimua kwa wanaume hao wazee ambao wengi wao hawana nguvu za kimapenzi hali ambayo imesababisha asilimia 40 kukutwa na maambukizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiana.