Wadhamini wa kombe la Dunia taabani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hadhi ya makampuni yanayothamini kombe la Dunia taabani Brazil.

Udhamini wa kandanda duniani umekua kwa kiasi kikubwa na sasa unazidi utoaji wa fedha kwa mashirika yanayoisimamia kwa shirika la soka duniani Fifa. Kinyume na hali ilivyokuwa hapo zamani wadhamini wanatumia mabango ya kielektroniki .

Uhusiano huu umekuwa mzuri zaidi .

Wdthamini wa kombe la dunia mwaka huu wanaelewa kuwa kuna ongezeko la hisia za watu kwa shirikisho hilo kutotawalwa na biashara pekee bali wajishirikishe na maswala ya kijamii na kisiasa katika maazimio yao ya kuthamini mashindano haya makubwa zaidi duniani.

Hili laonyeshwa kwa jinsi ambayo Sony imejishirikisha na mabishano yaliyotokea baada ya Qatar kutuzwa nafasi ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.

Adidas pia, wanaoidhamini michezo hii wanadai kuwa tukio hilo halikua zuri kwa kandanda, kwa Fifa na pia washiriki wake.

Mdhamini mwingine, Coca Cola amesema kuwa iko tayari kurudisha chini shughuli zake za kuitangaza kombe la dunia kwa sababu ya matukio ya fujo huko Brazil.

Makampuni na Wadhamini sasa wameibukia kuchangia maswala ya usimamizi kila wanapotoa hela zao na kama ilivyo bainika majuzi sasa wanamsukumo wa kujali hisia za jamii zinazoshirikiana katika michezo.

Hii ni kulingana na Nigel Currie, kutoka kwa Brand Rapport, ambayo ni kampuni ya kutathmini ufaulu wa makala ya michezo.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Wadhamini wa kombe la dunia taabani Brazil

Alisema kuwa wanaelewa kuwa kuna wale wenye malengo ya kudhuru, sio tu michezo yenyewe, bali pia makampuni yanayoifadhili michezo hiyo.

Wafadhili wanafaa kuwa tayari kwa matukio yoyote yatakayolenga kuwadhuru wao na bidhaa zao.

Michezo hiyo, ikiwa imesalia siku chache ianze, nchi zote 32 zinazo shiriki na pia wafadhili wote 22 wanafaa kujiandaa kimakini.

Na kulingana na mtaalam mmoja Brazili, wafadhili wale wakubwa wanajitahadhari katika haya yote.

Wafadhili wa Fifa Duniani

Wengi wanazidi kuwalimbikizia wafadhili hatia inayozingira fedha zinazotumika kwa sababu ya kombe hili la dunia.

Kwa hivyo kama ilivyo nchini Brazil Wafadhili hawaandai kampeini za kuhamasisha jamii kwa hofu kuwa huenda wakalengwa na watu wanaopinga sera za shirikisho la soka duniani FIFA na serikali ya Brazil.

''Shutuma hazifai kupewa Fifa na wafadhili wake, ila wanasiasa. Wafadhili wametoa hela nyingi ili kuhusishwa na kombe la dunia na hata ingawa wanatulia na kuwa walegevu, bado bidhaa yao itajulikana kote duniani.''anasema Nigel Currie

Katika kombe la dunia lililopita, afrika kusini, iliripotiwa kuwa ilitazamwa na Zaidi ya watazamji bilioni 3.2 kote duniani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mbwebwe za kombe la dunia huvutia watazamaji wengi duniani.

Fifa pia imefaidika kwa kuuza hisa kwa kampuni zinazotaka kuhusishwa na michezo hiyo.

Fifa inakadiriwa kupata pauni milioni 850 kila miaka mine kutoka kwa Wafadhili.

Currie anadai kuwa ikiwa ratiba ya kufadhili michezo hii ingelikua ya kubadilisha wafadhili kila miaka minne, makampuni yatakuwa na shauku kuhusu kushirikishwa kwao.

Kwa hivyo, kuna makampuni hususan kama vile Coca Cola, Hyundai/Kia, visa na Adidas, yasiyobadilishwa kwa muda mrefu.

Hata hivyo, la muhimu kwa wafadhili itakua kuwafanya wapenzi wa soka kutumia pesa zao zaidi katika kununua bidhaa za wafadhili hawa.

Matumizi ya kidijitali itakua ya muhimu katika kombe hili la dunia ikitiliwa maanani kuwa Brazili ni mtumizi wa pili kwa ukubwa wa mtandao wa Facebook na pia Youtube.