Refarii alituoonea Croatia Kovac

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Niko :Croatia ilidhulumiwa na hiyo penalti

Kocha wa Croatia Niko Kovac amesema kuwa hakuna faida ya timu yake kusalia brazil haswa baada ya timu yake kuambulia kichapo cha mabao 3-1 na Brazil katika mechi ya ufunguzi .

Kovac aliudhika sana na kauli ya refarii wa mechi hiyo Yuichi Nishimura ya kumwadhibu Dejan Lovren kwa kadi ya njano na kisha kuipa Brazil mkwaju wa adhabu hata baada ya kumgusa Fred katika mshikeshike ya kuwania mpira ndani ya eneo la lango la Croatia.

Neymar aliufuma kimiani mkwaju huo na kuiweka Brazil mbele kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo.

"haiwezi kuwa hivi katika mechi yetu ya ufunguzi hii ni dhulma " alisema Kovac

Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari kwa upande alimsifu refarii huyo kutoka Japan kwa kauli hiyo.

Mamilioni ya watu hawakuona ila yeye. Ninaamini kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka na usemi wa mwisho iwapo ilikuwa ni penalti au la .

Haki miliki ya picha VIPCOMM
Image caption Scolari: Nimeitizama mara 10 na hiyo ni penalti

Nimetazama kanda ya tukio hilo mara 10 na nikashaishika kuwa kweli ilikuwa ni Penalti alisema Scolari.

Kovac anasisitiza kuwa penalti hiyo haikufaa kabisa .Na kama ilikuwa inafaa basi kheri tuendelee kucheza mpra wa vikapu wala sio kandanda . Ni haramu hiyo. Croatia ilinyanyaswa' alifoka kocha huyo.

Iwapo matukio kama hayo yatarudiwa basi tutashuhudia penalti bandia 100.

Ninaamini takriban mashabiki bilioni 2.5 kote duniani walioshuhudia mechi hiyo watakubaliana nami kuwa haikuwa penalti hiyo.