Utumiaji wa dawa za kulevya A.Magharibi

Pendekezo limetolewa katika kanda ya Afrika Magharibi kuwa watu wanaopatikana na hatia ya kutumia viwango vidogo vya madawa ya kulevya wasichukuliwe hatua kali za kisheria.

Tume ya kupambana na madawa ya kulevya katika kanda hiyo, inasema kuwa makundi ya walanguzi yanahujumu eneo hilo kwa kulifanya kuwa kituo cha kulangua dawa za kulevya kama Cocaine.

Tume hiyo inayoongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, inasema kuwa walanguzi hao wanapaswa kukabiliana na walanguzi wala sio kuwaadhibu watu wanaotumia dawa za kulevya.

Kadhalika tume hiyo inasema kuwa sera za sasa zinachochea zaidi ufisadi na ghasia.

Ulanguzi wa dawa za kulevya na utumiaji wa dawa hizo limekuwa swala kubwa katika kanda ya Afrika Magharibi tangu mwanzo wa mwongo huu.

Juhudi za kupambana na ulanguzi wa Cocaine kutoka katika mataifa yanayozalisha mmea wa Coca Amerika ya Kusini hadi kwa watumiaji Marekani na Ulaya, zimesababisha wahalifu kulenga Afrika Magharibi kama mkondo mpya wa kusafirishia dawa hizo za kulevya.

Ripoti hiyo iliyopendekezwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, inaonyesha kwamba biashara ya Cocaine pekee kupitia kanda hiyo ina thamani ya dola bilioni 1.25. Pesa hizi ni nyingi kuliko pato la kitaifa la kanda nzima.