ICC yasema ina ushahidi dhidi ya Gbagbo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo

Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imesema kuwa ina ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka ya uhalifu wa kivita rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.

Anatuhumiwa kwa mauaji, ubakaji, jaribio la mauaji na udhalimu

Takriban watu 3,000 waliuawa nchi hiyo ilipotumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya bwana Gbagbo kutokabali kushindwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba, 2010.

Bwana Gbagbo mwenye umri wa miaka 69 ambaye ndiye Rais mstaafu wa kwanza kushitakiwa katika mahakama ya ICC anasisitiza kuwa hana hatia yoyote.

Anasema kuwa yeye ni mwathiriwa wa njama ya wakoloni wa zamani wa Ufaransa kumtoa uongozini

Majaji watakaoendesha kesi hiyo waliamua kuwa upande wa mashitaka haukuwa na ushahidi wa kutosha kumshutumu bwana Gbagbo lakini tarehe bado haijapangwa

Alikuwa rais wa Ivory Coast kuanzia mwaka 2000 hadi mwezi wa Aprili 2011 alipokamatwa na wanajeshi watiifu kwa rais Alassane Ouattara aliyeungwa mkono na askari wa kifaransa

Bwana Gbagbo ndiye rais mstaafu wa kwanza kukamatwa na kuwekwa kizuizini na mahakama ya ICC ingawa Slobodan Milosevic kutoka Yugoslavia na Charles Taylor kutoka Liberia walihukumiwa katika maalum Hague