Wito watolewa washia wajihami Iraq

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mamia ya vijana wameanza kukusanyika kwenda kupigana dhidi ya wasunni

Kiongozi wa waumini wa madhehebu ya kishia ametoa wito kwa wananchi kujihami tayari kwa vita dhidi ya wapiganaji wa madhehebu ya Kisuni wanaoendelea kuteka miji zaidi.

Wito huo uliotolewa na mwakilishi wa kiongozi wa washia Ayatollah Ali al-Sistani, ulikuja wakati wa maombi ya ijumaa huku wanamgambo hao wakiendelea kudhibiti maeneo ya kaskazini na mashariki na kutishia kuelekea kusini.

Umoja wa mataifa unasema kuwa mamia ya watu wamefariki huku wanamgambo hao wakiendeleza mauaji ya raia mmoja baada ya mwengine huko Mosul.

Marekani na Iran wameapa kusaidia katika vita dhidi ya wapiganaji hao.

Wakiongozwa na utawala wa kiislamu ,Iraq na kundi la (ISIS), wapiganaji hao wanatishia kufika hadi mji mkuu Baghdad na maeneo ya kusini yanayomilikiwa na wakaazi wengi wa kishia na miji mitakatifu ya Najaf na Karbarla ambayo inawachukulia kuwa kafiri.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maelfu wameanza kutoroka makwao kwa hofu ya usalama wao

Wakaazi wengi wa Iraqi hawana imani na jeshi la nchi hiyo baada ya wanajeshi kuhama.

Wapiganaji wa (ISIS)wameshinikiza watu kujiunga na makundi haramu ili kutetea miji na maeneo takatifu.

Wakati akihubiri kwenye maombi ya ijumaa huko karbala,Sheik Abdulmehdi al-Karbalai alisema raia wanaoweza kutumia zana za vita na kupigana didhi ya ugaidi, kutetea nchi yao,watu na maeneo takatifu, wanafaa kujitolea kujiunga na jeshi la usalama ili kutekeleza wajibu huo takatifu.

Mwanahabari wa BBC Richard Galpin anasema kuwa kuna ripoti kuwa maelfu ya watu tayari wameshajiunga na jeshi la mgambo la shia ambapo huenda wakachangia pakubwa katika utetezi wa Baghdad.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Barack Obama amezungumzia uwezekano wa kutuma wanajeshi wa Marekani Iraq

Wanamgambo hao wanapoelekea mashariki mkoa wa Diyala,katika eneo la mpakani na Iran walikabiliana na wanamgambo wa shia ,eneo la Udhaim takriban km 90 Kaskazini mwa Baghdad na Muqdadiya,km80 Kaskazini- Mashariki mwa jiji kuu.

Rais Hassan Rouhani wa Iran akiongea na waziri mkuu wa Iraqi Nouri Maliki hapo alhamisi alimhakikishia kuwa Iran haitakubali usalama na uthabiti wao kudidimia kupitia vitendo vya ugaidi

kulingana na jarida la wall street ambapo lilinukuu watu wasiojulikana,Iran tayari imetuma kikosi cha watu wawili kutoka jeshi la wanamgambo la al-Quds ili kusaidia serikali ya ya Iraqi.