Azma ya kumaliza ubakaji vitani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Angelina Jolie kwenye mkutano wa kujadili swala la ubakaji vitani uliofanyika mjini London

Kongamano kuhusu dhuluma ya ubakaji katika mataifa yaliyo katika mizozo ya kivita, imemalizika hii leo jijini London.

Huku mchezaji sinema wa Hollywood Angelina Jolie, akiwapongeza viongozi mbalimbali wa kiume duniani ambao wamejiandaa kukabiliana na itikadi za kale zilizopitwa na wakati.

Bi Jolie, ambaye pia ni balozi maalum wa shirika la umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi, amesema kuwa kukabiliana na swala hilo kutaboresha maisha ya wanawake waliomo katika maeneo ya mizozo.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry kwa upande wake amesema kuwa inawezekana kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kama silaha ya vita.

Wajumbe kutoka zaidi ya mataifa mia moja wamekuwa wakijadiliana jinsi ya kukomesha ukatili na ubakaji wakati wa makabiliano ya kivita.

Wameelezewa matukio mbali mbali ya wanawake waliodhulumiwa kimapenzi.

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya ICC, Fatou Bensouda aliambia kongamano hilo kuwa walikuwa katika sehemu mpya ya kihistoria

Matendo ya ubakaji yaweza kukomeshwa kwa ushirikiano wa washika dau wote.