Cameroon yanyamazishwa na Mexico

Image caption Matumaini ya Cameroon kufuzu hatua ya 2 yadidimia

Mexico yimejikita katika nafasi ya pili ya Kundi A nyuma ya Brazil baada ya ushindi wa bao moja kwa nunge dhidi ya wawakilishi wa Afrika the Indomitable Lions ya Cameroon.

Mechi hiyo ndiyo iliyokuwa ya pili baada ya ushindi tata wa Brazil dhidi ya Craotia hapo jana.

Kama mechi hiyo ya ufunguzi iliyoshuhudia maamuzi tata, Mabao mawili ya mshambulizi wa Giovanni Dos Santos yalifutiliwa mbali kutokana na kile wachambuzi wa mechi waliashiria kuwa ni makosa ya naibu wa refarii.

Licha ya hayo Mkwaju wa Dos Santos ulipanguliwa na kipa wa Cameroon kabla ya Oribe Peralta kufuma bao hilo la pekee na la ushindi kunako dakika ya 61 ya kipindi cha pili.

Cameroon itajilaumu yenyewe kufuatia matokeo hayo ambayo ilishindwa kufanya mashambulizi ila mkwaju wa Samuel Eto'o aliogonga mwamba huku kombora la Benoit Assou-Ekotto likipoteeza mwelekeo.

Kufuatia ushindi huo , Mexico ilisajili ushindi wake wa kwanza dhidi ya timu ya Kiafrika .

Kwa upande wao Cameroon waliongeza rekodi yao ya matokeo duni hadi kutimia mechi 14 bila ushindi.

Nusura Cameroon wasawazishe katika muda wa Majeruhi katika uwanja wa Estadio das Dunas ulioko Natal kombora la Benjamin Moukandjo lilipopanguliwa na kipa Guillermo Ochoa.

Kufuatia matokeo hayo sasa itawabidi Cameroon kujifunga kibwebwe na angalau kushinda mechi moja kati ya Brazil na Croati iliisonge mbele katika mkondo wa pil.