Uingereza yaahidi kusaidia Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekahu. Kundi lake linawazuia wasichana zaidi ya miambili

Uingereza imetangaza kuwa itaongeza msaada wake wa kijeshi na kielimu kwa Nigeria ili kuisadia katika juhudi za kupambana na kundi la wanamgambo la Boko Haram.

Hii ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.

Alisema kuwa jeshi la Nigeria litapokea mafunzo zaidi hususan katika kukabiliana na makundi ya wapiganaji wakati watoto zaidi ya milioni moja wakiwezeshwa kupata elimu.

Hii nido ahadi ya hivi karibuni ya nchi ya kimagharibi tangu kudi la wapiganaji wa Boko Haram kuteka nyara wasichana 200 wa shule mwezi Aprili.

Tangu utekaji nyara huo kufanyika , kundi hilo limezidisha mashambulizi yake nchini humo.

Kundi la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulizi tangu mwaka 2009 katika juhudi za kubuni taifa linalofuata sheria za kiisilamu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano ya kutaka wasichana waliotekwa nyara kuachiliwa

Maelfu ya watu wamefariki katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo na katika operesheni za jeshi kudhibiti ulinzi.

Bwana Hague amesisitiza kuwa haki za binadamu lazima ziheshimiwe katika operesheni yoyote dhidi ya wapiganaji hao.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yametuhumu jeshi la Nigeria kwa kuwaua mamia ya raia katika operesheni zao dhidi ya wapiganaji hao.

Waziri huyo kadhalika alisisitiza kuwa msaada uliotolewa lazima utumike kwa njia nzuri za kuwafaidisha wananchi na kuhakikisha kuwa jeshi linaendesha harakati zake vyema.