Uchunguzi Bomu Zanzibar

Haki miliki ya picha AP

Polisi visiwani Zanzibar wamewataka watu kuendelea kutoa ushirikiano ili kuweza kupata taarifa sahihi za watu wanaodaiwa kuhusika na shambulio la bomu lililotokea visiwani humo.

Taarifa za polisi Zanzibar zilizotolewa Afisa mwandamizi wa Mkadam Khamis zinaeleza kuwa hadi sasa uchunguzi aina ya bomu lililotumika na wahusika wa shambulio hilo.

Hivi sasa visiwani Zanzibar kuna mkutano mkubwa wa waumini wa dini ya Kiislamu kutoka katika nchi za Afrika mashariki hali ambayo inatia shaka kwamba huenda ndiyo walengwa wa shambulio hilo.

Katika miaka ya hivi karibuni Zanzibar imekumbwa na mashambulio ya mabomu yanayolenga viongozi wa dini, watalii na nyumba za ibada.

Mwezi februari mwaka huu shambulio jingine la bomu lilitokea katika kanisa la Anglican karibu na eneo la stone town lakini hakukua na maafa.