UNICEF;Watoto waathirika zaidi C.A.R

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa mataifa linalosimamia watoto UNICEF limeonya kuwa ghasia zinazoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati zinawaathiri pakubwa watoto.

Shirika hilo limesema kuwa takriban watoto 74 wamefariki huku wengine mia mbili na sabini na saba wakifanywa kuwa vilema katika kipindi cha miezi sita iliopita.

Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Soulaymane Diabate ameelezea ghasia hizo kama mbaya zaidi kutokana na ukatili wake.

Amesema kuwa mtoto mmoja ameuawa ama kulemazwa kila siku katika kipindi cha miezi sita iliopita.

Amesema kuwa zaidi ya watu laki mbili wameachwa bila makao.