Bomu la misumari lauwa mmoja Zanzibar

MJi mkongwe, Zanzibar

Mtu mmoja ameuwawa huku wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la bomu kisiwani Zanzibar.

Baadhi ya waathiriwa walikuwa wanaondoka katika msikiti mmoja ulioko katika maeneo ya mji mkongwe, mjini Zanzibar.

Haijulikani ni nani aliyefanya shambulio hilo ambalo lilijiri mkesha wa sherehe za kimataifa za filamu katika kisiwa hicho; na piya wakati kuna kongamano ya viongozi wa dini ya Islamu katika Afrika Mashariki, likifanyika huko.

Mwandishi wetu nchini Tanzania amezungumza na Insepekta Mkuu wa Zanzibar, Mohammed Mhina, ambaye amemwambia kuwa bomu liloripuka lilikuwa na misumari.

Hilo ni shambulio la pili la bomu mwaka huu.

Mwezi February mabomu mawili tofauti yaliripuliwa nje ya kanisa Anglikana, mji mkongwe, pamoja na mkahawa uliokuwa karibu na kanisa hilo.

Kumekuwa na hali ya wasiwasi wa kidini katika kisiwa hicho.