Iraq yawazuia wapiganaji kusonga mbele

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Iraq wakifyatua mizinga dhidi ya wapiganaji

Wanajeshi wa serikali ya Iraq pamoja na wanamgambo wa Kishia wameikomboa miji kadha kutoka kwa wapiganaji wa Kisunni ambao wamekuwa wakidhibiti maeneo ya kaskazini mwa nchi katika siku chache zilizopita.

Lakini miji muhimu ya Tikrit na Mosul bado iko mikononi mwa wapiganaji.

Mwandishi wa BBC anasema inaonesha wapiganaji hawakusonga mbele zaidi.

Na mripuko katikati ya Baghdad umeuwa watu kama 9 na kujeruhi kama 20.

Na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, amesema ghasia zinazotokea Iraq ni kwa sababu mataifa ya magharibi hayakuingilia kati nchini Syria.

Bwana Blair alikanusha kuwa chanzo cha ghasia za Iraq ni uvamizi uliofanywa na Marekani nchini Iraq, na ambapo yeye alikubali kushirikiana nayo mwaka wa 2003.

Lakini alikiri kuwa alikuwa na matumaini makubwa kuhusu hatima ya Iraq baada ya Saddam Hussein kung'olewa.