Iraq;Serikali yakomboa miji kadhaa

Haki miliki ya picha AP
Image caption wapiganaji wa kishia

Ripoti kutoka Iraq zinasema kuwa vikosi vya serikali pamoja na wanamgambo wa kishia wameyateka baadhi ya maeneo yaliodhibitiwa na wapiganaji wa kisunni kazkazini mwa Baghdad mbali na miji kadhaa kutoka kwa waasi hao.

Hatahivyo miji ya Tikrit na Mosul bado imesalia chini ya udhibiti wa wapiganaji hao .

Katika shambulizi moja kazkazini mashriki mwa mji mkuu,Ndege ya vikosi vya serikali iliwauwa wapiganaji saba wa kikurdi ambao walikuwa wanadhibiti eneo lililotorokwa na waasi wa kisunni.

Maafisa wamesema kuwa shambulizi hilo ni la makosa.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry awali aliiambia serikali ya Iraq kwamba usaidizi wa Marekani katika kukabiliana na wanapiganaji wa jihadi wa ISIS utafanikiwa iwapo viongozi wa Iraq wako tayari kuwacha tofauti zao.

Marekani inapeleka meli ya kubeba ndege katika eneo la Ghuba ili kukabiliana na ghasia nchini humo.