Saudi Arabia yakataza vibarua juani

Eneo la ujenzi, Qatar Haki miliki ya picha AFP

Sheria mpya za kazi zimeanzishwa nchini Saudi Arabia kwa watu wanaofanya kazi nje, kwenye jua.

Kutoka sasa hadi September, vibarua hawaruhusiwi kufanya kazi nje kutoka saa 6 mchana hadi 9 jioni, kwa sababu ya masilahi ya afya yao.

Wafanyakazi kwenye mitambo ya mafuta na kazi za lazima za ukarabati, hawahusishwi na uamuzi huo ikiwa hatua zinachukuliwa kuwakinga na jua.

Nchi jirani ya Qatar, imelaumiwa sana kwa kuwalazimisha vibarua kutoka India kufanya kazi kutwa nje, wakijenga mwahala mwa mashindano ya kandanda ya mwaka wa 2022.

Imesema itachukua hatua kufanya mazingira yao ya kazi kuwa bora.