Al Shabaab lakiri kushambulia Kenya

Image caption Watu zaidi ta arobaini na tano wameuawa katika mashambulizi ya Mpeketoni

Kundi la wapiganaji wa Al Shabaab nchini Somalia, limekiri kufanya mashambulizi katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu, Pwani ya Kenya.

Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu 49.

Huku wakikiri shambulizi hilo wametoa onyo kwa watalii kukoma kuja Kenya.

Taarifa ya kundi hilo ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi dhidi ya serikali ya Kenya kwa kufanya msako dhidi ya waisilamu kwa njia ya kuwafunga kiholela na kuwaua wahubiri wa kiisilamu.

Baadhi ya walioshuhudia mashambulizi hayo wamearifu BBC kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.

Image caption Mji wa Mpeketoni uko umbali wa kilomita miamoja kutoka eneo la mpakani na Somalia

Kenya imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al Shabaab tangu ipeleke wanajeshi wake Somalia mwaka wa 2011.

Duru kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa wapiganaji hao walifika katika malori mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha wakakivamia na kuiba silaha.

Pia waliteketeza hoteli na vijiji huku wakiwapiga watu risasi kiholela.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii