Ghana 1-2 Marekani

Image caption Mashabiki wa Marekani washangilia timu yao dhidi ya Ghana

02:57 Marekani imeshinda kwa mara ya kwanza katika mechi tatu za kombe la dunia dhidi ya Ghana .

02:56 Marekani imelipiza kisasi cha kushindwa katika michuano miwili ya kombe la dunia na Ghana .

02:56 Mpira umekwisha .

02:52 Ghana 1-2 Marekani

02:50 Dakika 5 za ziada .

02:49 John Anthony Brooks anaiweka Marekani 2-1 kwa kichwa

02:49 GOOOOOOOOAL

02: 48 Kona kuelekea Ghana

02:45 Andrew Ayew aisawazishia Ghana 81''

02:44 Ghana 1-1 Marekani

02:43 GOOOOOOOAL

02:35 Offside, Daniel Opare anammegea Kevin-Prince Boateng pasi safi lakini ameotea.

02:31 Mohammed Rabiu anaondoka .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bao la pekee kufikia sasa la Dempsey dakika ya 1

02:31Michael Essienanaingia uwanjani zikiwa zimesalia dakika 20 mechi hii ikamilike .

02:31 Ghana imemiliki mpira asilimia 60% Marekani 40 %

02:29 Kona kuelekea lango la Ghana

02:28 Kevin-Prince Boateng atuma mkwaju juu ya lango

02:26 Marekani inazidi kuhimili wimbi baada ya wimbi ya mashambulizi ya Ghana.

02:26 Marekani 1-0 Ghana 66''

02:25 Kona kuelekea lango la Marekani

02:24 Gyan anafuma mkwaju ambao unapanguliwa na Tim Howard .

02:21 Matokeo bado ni Marekani 1-0 Ghana dakika ya 60''

02:20 Andrew Ayew anatuma mkwaju unaopaa na kwenda nje

02:19 Badiliko :Kevin Prince Boateng anachukua nafasi ya Ayew

02:17 A. Gyan apoteza nafasi nzuri ya kuiswazishia Black Stars

Image caption Ghana iliwahi kuishinda Marekani mara 2 je watawahi mara hii

02:12 Gyan achezewa visivyo na inakuwa freekick

02:11 Germaine Jones ahimili mashambulizi ya Ghana ndani ya eneo

02 :07 A. Gyan anapigwa mweleka nje ya eneo na ni Freekick kuelekea lango la Marekani.

02:07 Marekani 1-0 Ghana

02:07Mpira umeanza tena kipindi cha pili.

01:50 Kipindi cha kwanza kimekamilika Ghana 0- 1 Marekani

01:49 Marekani 1-0 Ghana

01:48 Sulle Muntari anakanyagwa kichwa lakini refarii anasema si hoja mechi iiendelee

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashabiki wa Marekani washangilia bao la Dempsey

01:45 Kona kuelekea upande wa Ghana

01:45 Dakika 5 za ziada ya kipindi cha kwanza

01:39 Marekani inaongoza Ghana 1-0 kunako dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza

01:39 André Ayew (Ghana) aangushwa nje ya eneo

01:23 Jozy Altidore anaondolewa uwanjani kwa machela.

01:21 Altidore ananguka chini akishika paja la kushoto

01:15 Black stars inatafuta bao la kusawazisha baada ya Dempsey kuwatamausha na bao la sekunde ya 30 ya dakika ya kwanza .

01:15 Asamoa Gyan ajiangusha mbele ya lango akiwa amesalia na kipa pekee

01:13 Offside Ghana. André Ayewautuma mpira mbele ya lango lakini , Christian Atsu anasemekana ameotea

01:06 Marekani 1-0 Ghana dakika ya 5''

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ghana inatafuta ushindi dhidi ya Marekani

01:02 Marekani kabla ya leo imepoteza mechi mbili dhidi ya Black stars ya Ghana.

01:01 Marekani inafunga bao lake la kwanza kupitia kwa Clint Dempsey chini ya sekunde 30 tangu kipenga cha kuanza kwa mechi hii.

01:00 GOOOOOOOOAL !

01:00 mpira umeanza Ghana 0-0 Marekani.

Image caption Mashabiki wa Ghana kabla ya mechi dhidi ya Marekani

00:58 Ghana ilipopoteza mechi ya kufuzu kwa nusu fainali baada ya Luiz Suarez kushika mkwaju uliokuwa unaelekea kimiani.

00:56 Hakuna anayeweza kusahau matukio yalioikumba Black stars ya Ghana katika mchuano wa 2010 Afrika Kusini.

00:55Black stars ya Ghana inafungua kampeini yake ya Brazil 2014 dhidi ya Marekani katika uwanja wa Estadio das Dunas ulioko Natal