Je waijua siri ya Ivory.C kwenye Soka?

Image caption Vijana hufunzwa soka wakiwa wadogo na kukuwa wakiingia katika vilabu mashuhuri duniani

Timu ya Ivory Coast ni moja kati ya timu za Afrika zilioanza vizuri katika michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Brazil mwaka huu kwa kuonyesha uwezo wake dhidi ya Japan baada ya kuichabanga mabao 2-1.

Katika taarifa yake baada ya kutembelea taasisi ya michezo kwa vijana nchini humo mwandishi wa BBC Tamasin anagundua siri ya kwanini wachezaji wa Ivory Coast wanacheza kwa viwango vya kuridhisha katika michuano hii.

Issa Traore ni kijana mwenye miaka 16 anayesoma katika kituo maalumu cha michezo ya ASEC Mimosifcom Abidjan.

Wachezaji wengi wa kimataifa kutoka nchini humo, walipitia katika kituo hiki na Issa amejiunga akiwa na miaka 15.

Ni moja ya vituo vyenye mafanikio makubwa kati ya shule za michezo. Yeye anazungumza na mwandishi wa BBC Tamasin anayefuatilia siri ya mafanikio katika soka na maandalizi ya wachezaji tangia wakiwa wadogo.

'Soka kimataifa'

Image caption Ivory Coast inachanganya masomo na michezo ili kukuza vipaji vya vijana

Katika mazungumzo yake Traore anasema anajisikia mwenye bahati kuwa katika shule hiyo ya michezo kwani ndoto yake ni kuwa mchezaji mkubwa na mwenye mafanikio kama Yaya Toure, lakini pia anasema wazazi wake walipo mtembelea siku moja katika kituo hicho walifurahishwa sana na mazingira ya shule hiyo.

Miaka mitatu iliyopita Julien Chevalier alijiunga katika kituo cha cha michezo cha ASEC Mimosifcom kama kocha anasema kituo hiki kimekuwa na ufanisi mkubwa na kutoa wachezaji wakubwa kwani tangia kuanzishwa kwake 1994 Asec imetoa wachezaji wanao ng’ara kimataifa na kidunia.

Hata hivyo baadhi ya wahitimu wa miaka ya hivi karibuni tayari wanawika katika soka la ulaya ambao ni kama Anderlecht's Gohi, Bi Cyriac ,Saint-Etinne's na Ismael Diomande.

'Ukuzaji wa vipaji'

''Kila mwaka kituo hiki kimekuwa kikisajili watoto wapatao 7000 toka maeneo mbalimbali nchini humu hapo tunatarajia kutengeneza akina Drogba wa siku zijazo’’,anasema Chevalier huku akitabasamu.

Zaidi ya nusu ya wachezaji wanaocheza katika kombe la dunia ndani ya kikosi Ivory Coast o wamelelwa katika kituo hicho cha michezo cha Asec, hali ambayo inatajwa kuwawezesha kucheza mpira wenye ustadi zaidi.

Image caption Baadhi ya wachezaji wa kimataifa kama Yaya Toure wamepitia katika taasisi hiyo

Ni wachezaji wachache tu wa kimataifa toka Ivory Coast ndio ambao hawajapitia katika vituo maalumu vya michezo akiwemo Didier Drogba.

Hivyo siri kubwa na mafanikio ya soka nchini Ivory Coast ni pamoja na elimu ya kawaida ya darasani lakini bado vijana wamekuwa wakifanya bidii katika somo la kiingereza,Hesabu na kifaransa ,ambao wao wanasema masomo hayo ya lugha ni kwaajili ya kuwasaidia kwenda kuishi ulaya watakapokuwa wachezaji wa kimataifa.

Lakini pia utaratibu wa masomo nchini humo unawapa watoto fursa ya kushiriki michezo na kukuza vipaji vyao.