330 wafariki kutokana na Ebola

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu zaidi ya 300 wamefariki kutokana na Ebola

Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola Mgharibi mwa Afrika umesababisha vifo vya watu 330 tangu mwezi Februari.

Takwimu hizo mpya zilizotolewa na shirika la afya duniani WHO zinaashiria kuwa maafisa wa afya wanajaribu kuudhibiti ugonjwa huo.

Mlipuko huo uliofafanuliwa na shirika hilo kuwa mojawapo yalio mabaya zaidi ulianza nchini Guinea.

Umeenea pia hadi Sierra Leone na Liberia.

Takriban visa 50 vipya vimeripotiwa wiki iliyopita. Hakuna chanjo dhidi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola, vinavyosababisha mtu kuvuja damu kwa wingi na kuwa na joto jingi mwilini.