India, mteja mkubwa wa mafuta ya Nigeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kiwanda cha mafuta nchini Nigeria

Serikali ya Nigeria inasema kuwa India imekuwa nchi inayonunua mafuta ghafi kwa wingi kutoka kwake kuliko Marekani karibu robo ya mafuta yote kutoka nchini humo.

Kampuni ya kitaifa yua mafuta ya Nigeria inasema kuwa China na Malaysia zilinunua mafuta yake mengi kuliko Marekani. Marekani ndio ilikuwa mteja mkubwa wa mafuta kutoka kwa Nigeria katika miaka ya nyuma.

Nchi hiyo hununua takriban mitungi 250,000 ya mafuta kutoka nchini Nigeria kila siku.

Hitaji la mafuta kutoka kwa Marekani limeshuka sana kwa sababu ya ongezeko la uzalishaji wake wa mafuta.

Utabiri kutoka kwa makampuni ya mafuta ya BP pamoja na shirika la kimataifa la kawi unaonyesha kuwa Marekani huenda ikakidhi pakubwa hitaji lake la mafuta bila kununua kutoka nje kufikia mwaka 2035.