Ndege zisizo na rubani kutumiwa Mali

Image caption Hali nchini Mali bado ni tete kwani usalama bado haujapatikana tangi vita kuanza

Ndege zisizo na rubani zitaanza kutumiwa na Umoja wa Mataifa nchini Mali kukabiliana na utovu wa usalama eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Mkuu wa kikosi cha usalama cha Umoja huo, aliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa watasadia serikali kuwalinda raia.

Kikosi cha wanajeshi 8,000, wa Umoja huo kipo nchini humo kujaribu kuleta utulivu baada ya wanajeshi wa Afrika kuwatimua wapiganaji wa kiisilamu kutoka katika miji mikubwa 2013.

Waasi wa Tuareg bado wanaendesha harakati zao katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Mali,Abdoulaye, alisema kuwa serikali ingependa huduma za ndege zisizo na rubani kuanza haraka iwezekanavyo.

Baada ya vita mjini Kidal mwezi Mei, makundi matatu ya waasi wa Tuareg yalikubaliana kusitisha vita.

Bwana Ladsous alisema kuwa ndege hizo, zitatumiwa kuimarisha usalama na kuhakikisha kuwa raia wa kawaida wanapata ulinzi wa kutosha.

Pia alisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya amani na kudhibiti hali ya usalama ambayo inaendelea kudorora.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii