Taylor hataki kufungwa jela Uingereza

Haki miliki ya picha c
Image caption Taylor alihukumiwa jela miaka 50 kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu

Rais wa zamani wa Liberia, ameanzisha harakati za kisheria kupinga amri ya kutumikia kifungo chake cha jela nchini Uingereza.

Taylor alifungwa jela kwa uhalifu dhidi ya binadamu na anakataa kutumikia kifungo hicho Uingereza akisema kuwa ananyimwa haki ya kufurahia maisha yake.

Charles Tayor anatumikia kifungo cha miaka hamsini jela kwa makosa ya ubakaji na kutumia watoto kama wanajeshi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.

Mawakili wake wanasema kuwa kuzuiliwa kwake nchini Uingereza kunakiuka haki za binadamu kwa sababu ni mbali sana na yumbani kwa familia yake kuweza kusafiri huko kumuona.

Wanasema kuwa badala ya kutumikia kifungo Uingereza, aruhusiwe kutumikia kifungo hicho nchini Rwanda, pamoja na wafungwa wengine waliohukumiwa na mahakama maalum ya umoja wa mataifa kuhusu Sierra Leone.

Pia wanasema anahofia kushambuliwa na wafungwa wengine katika gereza la Frankland, Kaskazini mwa Uingereza.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii