Idadi ya wakimbizi yaongezeka duniani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wakimbizi wengi wametokana na vita vinavyoendelea nchini Syria

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, linasema idadi ya watu waliopoteza makao yao na kufanywa wakimbizi kutokana na vita ilizidi milioni hamsini mwaka jana.

Idadi hii inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.

Takriban watu milioni 17 walitoroka nchi zao na zaidi ya milioni thelathini ni wakimbizi wa ndani ya nchi zao.

Wengi wameishi katika kambi za wakimbizi kwa miaka mingi.

Athari za vita kwa watu

Milioni 51.2

watu walioachwa bila makao duniani

  • Milioni 2.6 walitoroka Afghanistan

  • Milioni 1.6 wanaishi nchini Pakistan

  • Milioni 1.2 wanatafuta hifadhi kote duniani

GETTY

Vita nchini Syria, ni moja ya sababu kuu ya kuongezeka kwa idadi hiyo ya wakimbizi, lakini pia kuna mizozo mingine katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na nchini Sudan Kusini ambayo imechangia idadi kubwa ya wakimbizi.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, linasema kuwa idadi hiyo ni ishara tosha ya athari za kukosa kuzuia mizozo. Pia limesema kuwa mataifa tajiri yanapaswa kufanya juhudi kuhifadhi wakimbizi hao.

Haki miliki ya picha BBC World Service