Malik:Serikali ya umoja haifai Iraq

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nouri Al Malik na John Kerry

Waziri mkuu nchin Iraq Nouri al Malik ameonya kwamba kubuni serikali ya umoja nchini humo ni mapinduzi dhidi ya katiba ya taifa hilo,na kuwa itaharibu mfumo wa demokrasia uliwekwa kufuatia kung'atuliwa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo marehemu Saddam Hussein miaka kumi na moja iliopita.

Marekani na mataifa mengine wamekuwa wakimshinikza waziri huyo mkuu kubuni serikali itakayoshirikisha wote kufuatia uchaguzi mwezio Aprili huku watu wa dhehebu la kisunni walio wachache na wale wa kikurdi wakiwakilishwa.

Hatua hiyo inajiri baada ya wanamgambo wa kisunni ISIS kuteka eneo kubwa la taifa hilo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Nouri al Malik

Nouri Al Malik alikuwa akizungumza katika runinga ya taifa hilo wakati wa hotuba yake ya kila wiki kwa taifa.

Lugha nzito aliyotumia kupinga wazo la serikali ya kitaifa wakati ambapo kuna tishio la wapiganaji wa kisunni ni onyo kubwa.

Bwana malik anaweka wazi kwamba atabuni serikali ya chaguo lake kwa kuwa ana haki kulingana na katiba kufuatia uchaguzi wake wa mwezi Aprili ambapo chama chake kilishinda kwa kura nyingi.

Matamshi yake yanaonyesha uwezekano kwamba serikali yake mpya ambayo nisharti ibuniwe mnamo mwezi Agosti haitakuwa ya uwakilishi kama inavyoshinikizwa na Marekani.