Makamu wa rais wa Argentina ashtakiwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Makamu wa urais wa Argentina Amado Boudou

Makamu wa rais nchini Argentina Amado Boudou ameshtakiwa na shtaka la ufisadi.

Bwana Badou anashtumiwa kwa kutumia vibaya mamlaka wakati alipokuwa waziri wa uchumi alipochukua umiliki wa kampuni inayochapisha fedha za Argentina.

Washukiwa wengine watana pia wameshtakiwa .

Bwana boudou kwa mara kadhaa amepinga mshtaka dhidi yake huku akifutilia mbali wito wa kujiuzlu.

Kwa sasa yuko katika ziara ya kibiashara nchini Cuba.