Serikai ya kijeshi kuunda bunge Thailand

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Thailand

Kiongozi wa jeshi nchini Thailand ametangaza bunge jipya ambapo wanajeshi wengi watachukua viti vingi litapobuniwa katika kipindi cha miezi miwili ijayo pamoja na serikali ya mpito.

katika hotuba yake kwa taifa kupitia runinga ya taifa hilo Jenerali Prayuth Chan Ocha pia amesema kuwa katiba mpya itaandikwa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao huku uchaguzi ukifanyika miezi mitatu baadaye.

Mwandishi wa BBC mjini Bangkok anasema kuwa Jenerali Prayuth aliweka wazi kwamba jeshi litashikilia mamlaka hadi wakati huo.

kumekuwa na shutma za kimataifa kuhusu mpango wa jeshi hilo kuimarisha demokrasia nchini humo baada ya kuipindua serikali mwezi uliopita.