Karne baada Vita vya Kwanza vya Dunia

Prince Franz Ferdinand na mkewe Haki miliki ya picha bbc

Shughuli zinafanywa leo kukumbuka tukio la karne kamili iliyopita mjini Sarajevo, ambapo mrithi wa mfalme wa mamlaka ya Austria-Hungary aliuliwa na mzalendo wa Serbia na kuwa chanzo cha kuzuka Vita vya Kwanza vya Dunia.

Vilembwe vya prince huyo, Franz Ferdinand, watahudhuria gwaride litalofanywa katika kasri yao karibu na Vienna, Austria.

Princess Anita Hohenberg, kilembwe cha Franz Ferdinand, aliiambia BBC kwamba Franz Ferdinand daima hakupenda vita:

"Baba wa babu yangu angeshtushwa, angeshtuka kabisa, kwa sababu akijua upungufu wa jeshi lake, kwa sababu alikuwa mkuu wa jeshi.

Vita hivo vilikuwa vibaya, vibaya sana."

Austria sasa haina mfalme.