Watu zaidi wahofiwa kufukiwa na kifusi

Image caption Jengo la makazi laporomoka Mumbai, India

Maafisa nchini India wamesema wanahofu kuwa zaidi ya watu 130 wamenasa kwenye kifusi cha jengo lililoporomoka kusini mwa India,takriban Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha katika tukio hilo mjini Porur.wengi wa walionasa wanaaminika kuwa wafanyakazi waliokuwa wakijenga jengo la ghorofa 11. Kikosi ha uokoaji kinafanya jitihada za kuokoa walioathiriwa na ajali hiyo. siku ya jumamosi, watu 10 ,miongoni mwao watoto watano, walipoteza maisha mjini Delhi,baada ya jengo la makazi ya watu kuporomoka. India imekua ikikumbwa na matukio ya kuporomoka kwa majengo, sababu ikielezwa kuwa usalama usio madhubuti na ujenzi usiozingatia viwango bora. Mwezi Januari mwaka huu, takriban watu 14 walipoteza maisha baada ya jengo lililokuwa kwenye hatua za ujenzi kuporomoka katika jimbo la Goa. Takriban watu 42 walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na Jengo la ghorofa nne mjini Mumbai mwezi Septemba mwaka jana.