Israel yatekeleza mashambulizi Ghaza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Israel

Israel inasema kuwa imetekeleza mashambulizi ya roketi katika eneo la Ghaza siku ya jumamosi ili kujibu shambulizi jengine la roketi kutoka kwa wapiganaji wa kipalestina.

Jeshi la Israel limesema kuwa limeshambulia kile ilichokitaja kama maeneo tisa ya ugaidi.

Awali roketi mbili zilipiga kiwanda kimoja katika mji wa Sderot nchini Israel na kukichoma mbali na kuwajeruhi watu wanne.

Mashambulizi hayo yanajiri wakati ambapo kuna wasiwasi huku wanajeshi wa Israel wakiendelea kuwasaka vijana watatu ambao walitoweka na wanaaminika kutekwanyara katika eneo la West Bank.

Israel inasema kuwa walitekwanyara na watu wa kundi la Hamas ambalo linadhbiti eneo la Ghaza.