Libya:Mshukiwa wa shambulizi mahakamani

Image caption Ahmed Abu Khatallah

Mmoja ya washukiwa wakuu wa shambulizi lililomuua balozi wa Marekani nchini Libya miaka miwili iliopita amefika mbele ya jaji katika mahakama moja ya kijimbo mjini Washington, Marekani.

Ahmed Abu Khatallah alikana mashtaka yote matatu ya ugaidi dhidi yake.

Mashtaka hayo yalisomwa kwake kupitia mkalimani.

Anashtakiwa kwa mauaji ya balozi Christopher Stevens pamoja na maafisa wengine watatu wa Marekani katika shambulizi la ubalozi wa Marekani mjini Benghazi.

Mshukiwa huyo alikamatwa na vikosi maalum na kusafrishwa kutoka Libya katika meli ya wanamaji wa Marekani.