Waangalizi waane waachiliwa Ukraine

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mmoja ya waangalizi

Shirika la usalama na ushirikiano wa ulaya limesema kuwa wapiganaji wanaounga mkono Urusi mashariki mwa Ukraine wamewaachilia waangalizi wengine wanne ambao walikuwa wametekwa nyara mwezi mmoja uliopita.

Wanne hao walikuwa wanazuiliwa katika mji wa Luhansk.

Siku ya ijumma wapiganaji hao waliwaachilia waangalizi wanne ambao walikuwa wamekamatwa katika mji wa Donestsk.

kwengineko, Mashambulizi ya wapiganaji wanaounga mkono Urusi yameendelea mashariki mwa Ukraine licha ya hatua ya serikali siku ya ijumaa kuongeza mda wa kusitisha vita hadi siku ya jumatatu.

Msemaji wa jeshi la Ukraine amethibitsha kuwa mwanajeshi mmoja wa serikali aliuawa nje mji wa Sloviansk ijapokuwa ripoti nyengine zinadai kuwa huenda idadi ya wanajeshi waliofariki ikawa juu.