Urasimu bandarini Mombasa kushughulikiwa

Bandari ya Mombasa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bandari ya Mombasa

Mashirika 25 yanayohudumu kazi katika Bandari ya Mombasa leo yanatia saini mkataba wa ushirikiano unaolenga kupunguza hasara ya mabilioni ya dola itokanayo na urasimu katika Bandari hiyo.

Sherehe za kusainiwa kwa mkataba huo zitaongozwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Kumekuwa na utaratibu mrefu wa kusafirisha na kupokea bidhaa kutoka bandari ya Mombasa inayotegemewa na nchi za Afrika Mashariki na kati, hususan kwa shehena za mizigo kutoka mataifa ya ng'ambo.

Mkataba huo unaazimia kupunguza siku za ukaguzi wa shehena zinzoingia na kutoka kwenye bandarini hiyo, na kupunguza malalamiko ya wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kupitia bandari ya Mombasa.