Mgomo mkubwa wakumba Afrika Kusini

Haki miliki ya picha
Image caption Wafanyakazi hawa wanataka nyongeza maradufu ya mishahara yao

Wafanyakazi ambao ni wanachama wa chama kikubwa cha wafanyakazi nchini Afrika Kusini wameanza mgomo wakidai mishahara yao kuongezwa kwa kiwango kikubwa.

Wanachama hao wanataka mishahara kuongezwa maradufu kufuatia mfumuko wa bei nchini humo.

Chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa Chuma na wahandisi kinanasema kuwa zaidi ya wanachama wake laki mbili wanashiriki mgomo huo.

Watafanyazi hao walitarajiwa kufanya maandamano katika miji sita muhimu nchini humo.

Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya uchumi mgomo huo unatarajiwa kuwa pigo kubwa katika uchumi wa Afrika Kusini ambayo katika miaka ya hivi karibuni imekumbwa na migomo ya wafanyikazi katika sekta ya migodi na viwanda .

Mgomo huo unakuja baada ya mgomo mwingine uliodumu kwa miezi mitano wa wafanyakazi wa kampuni ya dhahabu nyeupe kumalizika juma lililopita.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii