18 wauawa katika mlipuko Nigeria

Image caption Uharibifu uliotokea baada ya shambulizi

Takriban watu 18 wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni mjini Maiduguri Kaskazini mwa Nigeria.

Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.

Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kufanya shambulio hilo.

Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambilizi ya mara kwa mara licha ya operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji hao

Mwandishi wa BBC Habiba Adamu toka mji mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela eneo hilo anasema kuna utata wa idadi ya waliouawa katika shambulio hilo kwani wakati wengine wakisema waliouawa ni watano wengine wanasema huenda idadi ya waliouawa ikawa ni zaidi ya hiyo iliyotolewa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii