Mapigano mapya yaripotiwa Iraq

Haki miliki ya picha Reuters

Mapigano mapya yameripotiwa kati ya kundi la Jihad la Sunni na majeshi ya serikali katika mji wa Tikrit nchini Iraqi. Watu walioshuhudia mapigano hayo wameona vumbi la milipuko ya mapigano hayo na kwamba makazi ya Rais wa zamani Saddam Hussein yameshambuliwa pia. Hata hivyo kuna taarifa kwamba waasi hao wananshikilia baadhi ya ngome za kijeshi katika mapambano hayo. Tikrit ni mji ambao umekuwa ukishikiliwa na wanajeshi wa Isis tangu 11mwaka huu ambapo walifanikiwa kujiimarisha Kaskazini na magharibi mwa Iraq. Rais wa Marekan Barack Obama ametangaza kupelekwa kiasi cha wanajeshi 200 kuimarisha usalama wa ubalozi wake mjini Baghdad. Bunge la Iraqi linatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza kuzngumzia hali hiyo tangu kufanyika kwa uchaguzi mwezi April. Waziri mkuu wa Iraq Nouri Maliki ana nia ya kuwania kipindi cha tatu cha uongozi wake japo kuwa waangalizi wa kimataifa wanamhusisha na machafuko ya sasa na kuona kwamba hafai kugombea tena. Kikosi cha wanajeshi 750 wa mMarekani kipo nchini Iraq kukabiliana na wapiganaji hao.