Ajali ya ndege yawaua wanne Kenya

Ajali ya ndege Nairobi
Image caption Shughuli za uokozi zikiendelea baada ya ndege ya mizigo kuanguka jijini Nairobi

Watu wanne akiwemo Rubani wa ndege moja ya mizigo, wamefariki dunia baada ya ndege walimokuwa kuanguka mapema leo asubuhi katika mtaa wa Embakasi jijini Nairobi.

Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba shehena ya Miraa ama Mairungi kuelekea Mogadishu nchini Somalia.

Uchunguzi umeonyesha kuwa ndege hiyo huenda iligonga mlingoti wa stima karibu na mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi na kuanguka.