Sokwe Rwanda kupewa majina leo!

Sokwe Haki miliki ya picha Stuart Christie
Image caption Sokwe wa milimani

Kwa kawaida Mtoto anapozaliwa katika familia yake huwa inaandaliwa sherehe ya kumpa jina .

Hata hivyo si jambo la kawaida katika tamaduni nyingi hasa za kiafrika kuandaa sherehe za kuwapa majina wanyama. Lakini nchini Rwanda leo zinatarajiwa sherehe kubwa ya kuwapa majina watoto wa sokwe wa milimani.

Sokwe hao ni kutoka mbuga ya wanyama ya Volcano kaskazini mwa taifa hilo. Sekta ya utalii hasa sokwe wa milimani ni ya kwanza kuingizia Rwanda fedha za kigeni.

Tukio la hilo la kuwapatia majina watoto wa Sokwe maarufu kama'' Kwita izina'' limeendela kupata umaarufu ambapo huhudhuriwa na wadau mbali mbali maarufu wa hifadhi ya wanyama pori kutoka nchi mbali mbali duniani.