Chupi za Afrika zinazosifika Ufaransa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Sampuli ya chupi zinazo shonwa na mafundi wa Copromof wakiwa kazini

Oscar Dao ni Fundi cherehani nchini Burkina Faso. Anashughulika kushona kile kinachomalizika kuwa chupi ya mwanamke ya rangi ya waridi.

"Ni furaha kubwa kutengeneza vitu vizuri kama hivi, vya kiwango cha juu," anatania fundi huyo mwenye miaka 36.

Akiendelea na shughuli kwenye cherehani chake katika duka la Copromof katika mji mkuu Ouagadougou, Fundi Dao anafanya mabadiliko taratibu.

Huku kukiwepo mzozo wa pamba magharibi mwa Afrika, na wakati kampuni za mitindo Ulaya zimehamisha utengenazaji bidhaa Asia, Kampuni ya kutengeneza chupi ya Ufaransa, Atelier Augusti imeamua kutengeneza nguo za ndani za wanawake Ouagadougou.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Therese Tiema pia hushona nguo binafsi kama sare za shule

Mmiliki duka hilo, Therese Tiema, ameajiri wafanyakazi watatu zaidi katika miaka miwili iliyopita - na kuiweka idadi ya mafundi cherehani aliyowaajiri kuwa tisa kati ya vyerehani 15, wanaoshona chupi zilizoagizwa na kampuni hiyo ya Ufaransa.

"bado tunashona nguo binafsi lakini tunajaribu kuondoka kwenye soko hilo na kuishia kupokea maagizo makubwa".

Kutoka Afrika hadi Ufaransa

Atelier Augusti ni kampuni inayomilikiwa na dada wawili Julie na Claudie Ramirez walioizuru Burkina Faso kwa mara ya kwanza miaka misita iliyopita baada ya mama yao kuolewa na raia wa huko.

"kwetu haikuwa uamuzi kati ya kutengeneza nguo hizi katika eneo la mashriki au Afrika," anasma Claudie Ramirez mwenye umri wa miaka 27.

"daima ilikuwa ni Afrika, licha ya kwamba ingekuwa rahisi kuzitengeneza katika eneo hilo la mashriki," anasema.

Ndugu hao wanataka chupi hizo zitengenezwe kwa kutumia pamba asilia ambaoyo huinunua kutoka kiwanda kikubwa cha nguo cha Comatexkatika nchi jirani ya Mali.

"Hatahivyo ni lazima tutume mipira na wino wa chaa ya kampuni kutoka Ufaransa. Kiwango tunachokihitaji hakipatikaniBurkina Faso."

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kila chupi hukatwa na kushonwa kivyake

Chupi hizo zinauzwa kwenye mtandao na pia katika maduka manne nchini Ufaransa likiwemo moja katika mji mkuu, Paris.

Claudie anasema kuuza chupi hizo Burkina Faso inakuwa vigumu kwa sababu bei yake ambayo ni dola 25, ipo juu zaidi ya bei ya chupi zengine zinazonunuliwa nchini humo.

Mmiliki wa duka la Copromof wanakoshona mafundi, Tiema anakubaliana na hilo: "sokoni unaweza kununua kwa bei rahisi chupi za kutoka China, lakini zina madhara kwenye ngozi."

"Nina hakika kungekuwa na soko kwa chupi zilizotengenezwa vizuri kwa pamba asili zilizonuiliwa miili ya Waafrika".