Uchumi wa Urusi Matatani-IMF

Image caption Matajiri wasemekana kuondoa fedha zao Urusi kwa sababu ya vikwazo

Shirika la fedha duniani IMF linasema kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi wa Urusi kimeshuka kuelekea sifuri,kufuatia vikwazo ilivyowekewa na Marekani na muungano wa Ulaya.

Shirika la fedha duniani IMF limesema kupigwa tanji kwa mali za Urusi na vikwazo vya Visa kwa baadhi ya wakuu wa taifa hilo, kufuatia kitendo cha Urusi kuimegua Crimea kutoka kwa Ukrain, ni baadhi ya matukio yaliyochangia kuporomosha imani ya waekezaji nchini Urusi.

Kutokana na hali hiyo katika kipindi cha miezi mitano ya mwanzoni mwa mwaka huu Urusi imekumbwa na hali ya wenye fedha kuondosha pesa zao kutoka taifa hilo zinazokadiriwa kufikia dola billion 80 US.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mpiganaji wa Urusi akiwa Ukraine- vikwazo vimechochewa na mzozo kati ya urusi a Ukraine

Hali ya wasiwasi katika kanda hiyo imefanya pia makampuni ya Urusi kuweza kupata mikopo kutoka masoko ya kimataifa.

IMF pia inasema mageuzi ya kupanua uchumi vilevile yametatizwa chaguo la Urusi la kuweka mkazo katika sera ya kujitegemea yenyewe kuliko ushirikiano na jamii ya kimataifa.

Hata hivyo maafisa wa kiuchumi wa Urusi wanasema wana imani taifa lao litaweza kushinda masaibu hayo yanayotishia uchumi wao na kutabiri uchumi huo utakuwa kwa angalau asilimia japo moja kufikia mwishoni mwa mwaka.