Wapalestina 10 wajeruhiwa ukanda wa Gaza

Image caption Kijana wa kipalestina Mohamed Abukhadair kuzikwa leo

Takriban raia kumi wa Palestina wameripotiwa kujeruhiwa kutokana na mfululizo wa mashambulizi ya anga katika eneo la ukanda wa Gaza,ambapo Jeshi la Israel linadai mashambulizi yalilenga vifaa vinavyotumiwa na wapiganaji wa Hamas na Islamic Jihad.

Israel imesema kuwa mashambulizi hayo ni majibu ya mashambulizi takriban ishirini ya Roketi yaliyotokea Palestina yakishambulia kusini mwa Israel kwa kipindi cha saa ishirini na nne.

Marekani imezitaka pande mbili kuchukua hatua kuzuia hali ya kulipiza kisasi baada ya kifo cha kijana wa kipalestina, mashambulizi yaliyotekelezwa siku moja baada ya mazishi ya vijana watatu wa Israel.

Kijana wa miaka kumi na saba Mohammed Abukhadair anazikwa siku ya alhamisi.