Mazishi ya kijana yaahirishwa palestina

Image caption Kijana wa kipalestina aliyeuawa Mohammed Abu Khdair

Mazishi ya kijana wa kipalestina aliyetekwa nyara na kuuawa mjini Jerusalem yameahirishwa kutokana na mgogoro kuhusu siku mwili wa kijana huo utakapokabidhiwa kwa familia.

Familia ya Mohammed Abu Khdair imesema Polisi wamekataa kuwapatia mwili huo, madai ambayo polisi imekanusha.

Kuuawa kwake kulileta hali ya wasiwasi hasa kutokana na madai kuwa lilikua tukio la kulipa kisasi baada ya kuuawa kwa vijana watatu wa Israel.

Israel ilitekeleza mashambulizi ya anga katika eneo la Gaza siku ya alhamisi dhidi ya wanamgambo.

Maafisa wa Israel wamesema wanamgambo walitekeleza mashambulizi ya roketi tangu asubuhi siku ya jumatano na kuharibu nyumba lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Maafisa kutoka Wizara ya afya ya Gaza wameiambia BBC kuwa wapalestina 10 walijeruhiwa katika shambulio la anga na kukimbizwa hospitalini.