Pistorius "anasumbuliwa na ulemavu"

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Oscar Pistorius

Mwanariadha wa Afrika Kusini asiye na miguu yote miwili Oscar Pistorius ameathirika vibaya kutokana na ulemavu wake, daktari wa michezo ameiambia mahakama inayosikiliza kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha huyo.

Wayne Derman ameiambia mahakama mjini Pretoria kuwa bingwa huyo wa olimpiki ameathirika vibaya "kutokana na msongo wa mawazo na hofu".

Bwana Pistorius anasema alimuua kwa kumpiga risasi rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp baada ya kumdhania ni mwizi aliyeingia ndani ya nyumba yao mwaka jana.

Upande wa mashitaka unasema kuwa Pistorius alimuua kwa makusudi Bi Steenkamp baada ya kuzozana.

Suala linaloangaliwa ni akili ya Pistorius wakati akifyatua risasi dhidi ya Reeva.