Liverpool kumuachia Suarez?

Haki miliki ya picha
Image caption Huenda Luis Suarez akaichezea Barcelona

Kaimu mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre aliutumia muda wake mwingi kwa majadiliano na maafisa wa juu wa Barcelona siku ya jumatano jijini London.

Liverpool imeshikilia msimamo wake kuwa Suarez 27, hatauzwa kwa kiwango cha chini ya kile wanachokihitaji kumuachia mchezaji huyo kinachoaminiwa kuwa kati ya Pauni milioni 70 na 80.

Afisa mmoja wa Liverpool ameiambia BBC kuwa mazungumzo yalizaa matunda na kuwa pande zote zina matarajio chanya. bado hawajafikia makubaliano hata hivyo mazungumzo zaidi yataendelea.

Suarez, aliyejiunga na Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 22.7 kutoka Ajax na ambaye amebakisha miaka mine kuichezea timu hiyo kwa mujibu wa mkataba wake, anatumikia adhabu ya kufungiwa kucheza soka kwa miezi mine baada ya kumng'ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellini katika mechi ya kombe la dunia.