Hamas kusitisha mashambulizi Israel

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa kundi la Hamas

Taarifa kutoka Gaza zinasema wapiganaji wa Palestina wa Hamas kimesema kipo tayari kusimamisha mapigano ya maroketi kwenye miji nchini Israel na kutaka kuhakikishiwa kuhusu mashambulio ya anga katika ukanda wa Gaza nayo yasitishwe mara moja.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yalikuwa yakisimamiwa na maafisa kutoka nchini Misri.

Israel imesema itapeleka vikosi zaidi vya majeshi yake katika mpaka wa ukanda wa Gaza, ili kujibu mashambulio ya maroketi yaliyofanywa na Palestina, ndani ya ardhi ya Nchi yake.

Katika maeneo ya mashariki mwa Jerusalem kumeshuhudiwa siku ya pili ya maandamano ya kupinga mauwaji ya kijana wa kipalestina. Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika hatimaye hii leo Ijumaa.

Hata hivyo maafisa wakuu wa Majeshi ya Israel wamesema hatua hiyo ni ya kujilinda na wala haina nia ya kuchochea machafuko zaidi kati yake na Palestina.