Watafiti watafsiri lugha wanayotumia Sokwe

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mawasiliano kati ya Sokwe ni sawa na wanavyowasiliana binadamu

Watafiti wanasema kuwa wameweza kutafsiri maana ya ishara za mawasiliano zinazotumiwa na Sokwe wanaoishi msituni

Wanasema kuwa Sokwe hao, huwasiliana kwa kutumia ujumbe 19 na kwa ishara 66.

Wanasayansi hao waligundua hili kwa kuwafuatilia na kuwanasa kwa video Sokwe nchini Uganda na kutathmini zaidi ya visa 5000 vya umuhimu wa mawasiliano hayo.

Matokeo ya utafiti huu yamechapishwa katika jarida la Bayolojia ya kisasa.

Daktari, Catherine Hobaiter, aliyeongoza utafiti huo, alisema kuwa huu ndio mfumo pekee wa kimataifa wa mawasiliano kuhusu wanyama kuwahi kurekodiwa.

Ni binadamu pekee na Sokwe ambao wana mfumo wa mawasiliano ambapo walitumiana ujumbe kwa lengo fulani

''Hicho ndicho kitu kimetushangaza sana kuhusu ishara zinazotumiwa na Sokwe katika mawasiliano yao,'' alisema mtaalamu huyo.

Hawa ndio wanyama pekee wanaosalia kuwa na mfumo sawa wa mawasiliano na binadamu. '' aliongeza daktari huyo.

'Mayowe au ishara?'

Ingawa utafiti ambao umefanywa hapo awali, umefichua kuwa wanyama hawa pamoja na Nyani wanaweza kuelewa lugha ngumu kutoka kwa kilio cha mnyama mwingine, wanyama hao hawaonekani kutumia sauti zao katika kutuma ujumbe huo.

Mwanzo Sokwe watahakikisha kuwa ujumbe umeweza kumfikia mnyama anayetakikana.

Hii ilikuwa tofauti kubwa kati ya kupiga mayowe na kutoa ishara kwa mnyama fulani, kulingana na daktari Hobaiter.

Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa inshara zinazotolewa na Sokwe, hazieleweki vyema , ingawa hizo ndizo hutumika zaidi kwa mawasiliano yao.

Mfano kula majani kwa wanyama hawa huwa ni ishara ya kutaka kujamiiana,

Haki miliki ya picha BBC World Service

Ingawa baadhi ya ishara hazieleweki, zile zilizonaswa kwenye kanda ya video zilionyesha ujumbe uliokuwa unawasilishwa.

Katika moja ya kanda ya video, Sokwe mama anamnyonyea mguu mtoto, ishara ya kumtaka kupanda katika mgongo wake ili watembee pamoja.

Sokwe ni wanyama wanaoonekana kuwa na ukaribu mkubwa na binadamu hasa kwa wanavyowasiliana.

Mmoja wa watafiti wa utafiti huo alisema kuwa utafiti wenyewe ulikuwa muhimu sana katika kutaka kuelewa mchipuko wa mawasiliano miongoni mwa binadamu.

Lakini alisisitiza kuwa matokeo hayakufichua mengi waliyoyataka.