Australia yawarudisha wakimbizi makwao

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boti la wakimbizi

Australia imedinda kutoa tamko kuhusu ripoti kwamba imezuia maboti mawili yaliokuwa yakiwabeba wakimbizi wa Tamil na badala yake ikaanza kuwakabidhi kwa wanamaji wa Sri-lanka.

Serikali imesema kuwa haiwezi kuzungumza kuhusu swala hilo kutokana na sababu za oparesheni zake,lakini mawaziri wamesisitiza kuwa taifa hilo linachukua jukumu lake.

Wana kampeni hatahivyo wanasema kuwa Australia linakiuka haki za kibinaadamu mbali na sheria za kimataifa.

Kuyazuia maboti ya wakimbizi kutofika nchini Australia ni miongoni mwa ahadi za kampeni zilizotolewa na waziri mkuu wa mrengo wa kulia Tony Abbot.