Bei ya mafuta yapandishwa sana Misri

Magari katika Medani Tahrir mjini Cairo Haki miliki ya picha bbc

Madereva wa taxi katika miji kadha ya Misri wameziba njia kulalamika juu ya hatua ya serikali ya kuongeza bei ya mafuta kwa kiwango kikubwa.

Kutoka Jumamosi bei ya mafuta imepanda kwa 78% kufuatana na tangazo lilotolewa Ijumaa jioni.

Bei ya umeme kwa jumla inapanda huku serikali inajaribu kukata fidia ili ipunguze kasoro katika bajeti na ifufue uchumi ulioumia katika mchafuko wa kisiasa.

Umeme unakatwa mara kadha nchini Misri, na wakuu wanasema ruzuku inayotoa serikali ndio sababu ya uzalishaji wa umeme na mitambo yake kutoshughulikiwa sawa-sawa.