Waziri mkuu wa Senegal apigwa kalamu

Haki miliki ya picha
Image caption Waziri mkuu wa Senegal Aminata Toure

Waziri mkuu nchini Senegal Aminata Toure ameachishwa kazi baada ya chama tawala kushindwa katika uchaguzi mkuu.

Maafisa wanasema kuwa Rais Macky Sall alimtaka kujiuzulu baada ya kuhudumu chini ya kipindi cha mwaka mmoja.

Waandishi wanasema kuwa kutorodhika kwa wanachi kuhusu sera za uchumi za serikali hiyo ndio sababu kuu ya chama hicho kushindwa katika uchaguzi huo.