Marekani yakasirishwa na hatua ya Israel

Image caption Ghasia kati ya Palestina na Israel

Marekani imesema kuwa ina wasiwasi mwingi kwamba maafisa wa Polisi wa Israel wamempiga vibaya kijana mmoja raia wa Marekani.

Idara ya maswala ya kigeni imesema kuwa inashtumu utumiji wa nguvu kupitia kiasi na kutaka uchunguzi wa haraka na ulio huru kufanywa .

Kijana huyo Tariq Khdeir ni binamu wa Mohammed Abu Khdeir ,kijana wa kipalestina ambaye mauaji yake mashariki mwa Jerusalem yamezua ghasia.

Polisi ya Israel inasema kuwa kijana huyo ni miongoni mwa raia sita wa kipalestina waliojihami ambao walikamatwa wakati wa ghasia hizo.

lakini baba ya kijana huyo anasema mwanawe hakuhusika kamwe.

Ghasia hizo zilienea hadi katika miji mingine ya kiarabu nchini Israel siku ya jumamosi kufuatia ripoti kwamba Mohammed Abu Khdeir alichomwa akiwa mzima.