Wapiganaji 53 wa Boko Haram wauawa

Haki miliki ya picha afp
Image caption Wapiganaji wa Boko Haram

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wanachama 53 wa kundi la Boko haram kufuatia shambulizi la wapiganaji hao katika mji wa kazkazini wa Damboa .

Limesema kuwa wanajeshi watano waliuawa katika vita hivyo vilivyoanza usiku wa siku ya ijumaa.

Maafisa wa eneo hilo hatahivyo wamesema kuwa idadi ya wanajeshi na raia waliouawa ni kubwa.

Wapinagaji hao waliojihami kwa silaha kali walikuwa wamelenga kambi moja ya kijeshi.

Kijiji cha Konduga kazkazini mashariki pia kinadaiwa kushambuliwa siku ya ijumaa.

Ripoti zinaarifu kwamba takriban watu watano wameuawa katika misururu ya mashambulizi ya kila siku.